Kiambishi ni kipande cha neno chenye maana ya kisarufi ambacho kinapachikwa kwa mfano kabla au baada ya mzizi wa neno katika vitenzi na kuwakilisha dhana fulani. [1]
Miongoni mwa viambishi vya Kiswahili mna NI, NDI, KI, KA na kadhalika.
Kiambishi kikitangulia mzizi au kiini cha neno kinaitwa kiambishi awali, kikifuata kinaitwa kiambishi tamati.