Kiarmenia

Maandishi ya Kiarmenia, karne ya 5–6.
Biblia ya kwanza kwa lugha ya Kiarmenia.

Kiarmenia ni lugha ya pekee katika jamii ya lugha za Kihindi-Kiulaya.

Kinatumiwa na watu milioni 6, hasa nchini Armenia (ambapo ni lugha rasmi) na kandokando yake.

Alfabeti yake maalumu ilibuniwa na Mesrop Mashtots mwaka 405.

Fasihi yake ina historia ndefu, ikianza na tafsiri ya Biblia ya karne ya 5.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne