Kiarop-Sissano ni lugha ya Kiaustronesia nchini Papua Guinea Mpya inayozungumzwa na Waarop-Sissano. Mwaka wa 1998 idadi ya wasemaji wa Kiarop-Sissano imehesabiwa kuwa watu 1150. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiarop-Sissano iko katika kundi la Kioseaniki.