Kias ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Waas kwenye kisiwa cha Papua. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kias imehesabiwa kuwa watu 230 tu. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kias iko katika kundi la Kiraja-Ampat.