Kiatemble ni lugha ya Kivuka-Guinea Mpya nchini Papua Guinea Mpya inayozungumzwa na Waatemble. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kiatemble imehesabiwa kuwa watu 60 tu, na lugha iko hatarini mwa kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiatemble iko katika kundi la Kiwanang.