Kiavikam

Kiavikam ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Cote d'Ivoire inayozungumzwa na Waavikam. Mwaka wa 1993 idadi ya wasemaji wa Kiavikam imehesabiwa kuwa watu 21,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiavikam iko katika kundi la Kikwa.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne