Kiayabadhu ilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Waayabadhu kwenye rasi ya Cape York katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kiayabadhu ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiayabadhu iko katika kundi la Kiwik.