Kibada ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wabada kwenye kisiwa cha Sulawesi. Isichanganywe na lugha ya Kibada izungumzwayo nchini Nigeria. Mwaka wa 1989 idadi ya wasemaji wa Kibada imehesabiwa kuwa watu 6800. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibada iko katika kundi la Kicelebiki.