Kibafanji ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Kamerun inayozungumzwa na Wabafanji. Mwaka wa 2008 idadi ya wasemaji wa Kibafanji imehesabiwa kuwa watu 17,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibafanji iko katika kundi la Grassfields ambalo linafanana na lugha za Kibantu.