Kibaka ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Kamerun inayozungumzwa na Wabaka. Isichanganywe na Kibaka cha Sudan. Mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kibaka nchini Kamerun imehesabiwa kuwa watu 40,000. Pia kuna wasemaji 3200 nchini Gabon. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibaka iko katika kundi la Kiadamawa-Ubangi.