Kibakumpai

Kibakumpai ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wabakumpai kwenye kisiwa cha Kalimantan. Mwaka wa 2003 idadi ya wasemaji wa Kibakumpai imehesabiwa kuwa watu 100,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibakumpai iko katika kundi la Kibarito. Kibakumpai hutumiwa kama lugha ya soko katikati ya kisiwa.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne