Kibali (Nigeria)

Kibali ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Nigeria inayozungumzwa na Wabali. Isichanganywe na lugha ya Kibali izungumzwayo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mwaka wa 1991 idadi ya wasemaji wa Kibali imehesabiwa kuwa watu 2000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibali iko katika kundi la Kiadamawa-Ubangi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne