Kibalochi-Mashariki

Kibalochi ya Mashariki ni lugha ya Kihindi-Kiulaya nchini Pakistan na Uhindi inayozungumzwa na Wabalochi. Mwaka wa 1998 idadi ya wasemaji wa Kibalochi ya Mashariki nchini Pakistan imehesabiwa kuwa watu 1,800,000. Pia kuna wasemaji 800 nchini Uhindi (2007). Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kibalochi ya Mashariki iko katika kundi la Kiiran. Huandikwa na alfabeti ya Kiarabu.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne