Kibamali ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Kamerun inayozungumzwa na Wabamali. Mwaka wa 2008 idadi ya wasemaji wa Kibamali imehesabiwa kuwa watu 10,800. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibamali iko katika kundi la Grassfields ambalo linafanana na lugha za Kibantu.