Kibambili-Bambui

Kibambili-Bambui ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Kamerun inayozungumzwa na Wabambili-Bambui. Mwaka wa 1983 idadi ya wasemaji wa Kibambili-Bambui imehesabiwa kuwa watu 10,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibambili-Bambui iko katika kundi la Grassfields ambalo linafanana na lugha za Kibantu.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne