Kibamukumbit ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Kamerun inayozungumzwa na Wabamukumbit. Mwaka wa 2008 idadi ya wasemaji wa Kibamukumbit imehesabiwa kuwa watu 12,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibamukumbit iko katika kundi la Grassfields ambalo linafanana na lugha za Kibantu.