Kibanda

Kibanda ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wabanda kwenye visiwa vya Kei. Kwa asili Wabanda wametoka kisiwa cha Banda lakini lugha ya Kibanda imeachwa kuzungumzwa huko. Mwaka wa 1987 idadi ya wasemaji wa Kibanda imehesabiwa kuwa watu 3000. Kwa vile Wabanda wengi wameanza kuacha lugha yao, Kibanda imekaribia kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibanda iko katika kundi la Kimaluku.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne