Kibanda-Bambari ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati inayozungumzwa na Wabanda. Mwaka wa 1996 idadi ya wasemaji wa Kibanda-Bambari imehesabiwa kuwa watu 183,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibanda-Bambari iko katika kundi la Kiadamawa-Ubangi.