Kibangandu

Kibangandu ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Kamerun inayozungumzwa na Wabangandu. Mwaka wa 1977 idadi ya wasemaji wa Kibangandu nchini Kamerun imehesabiwa kuwa watu 2700. Pia kuna wasemaji wachache nchini Jamhuri ya Kongo. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibangandu iko katika kundi la Kiadamawa-Ubangi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne