Kibati (Kamerun)

Kibati ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Kamerun inayozungumzwa na Wabati. Mwaka wa 1975 idadi ya wasemaji wa Kibati imehesabiwa kuwa watu 800 tu. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibati iko katika kundi la Kimbam ambalo linafanana na lugha za Kibantu.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne