Kibatuley (pia Kigwataley) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wabatuley kwenye visiwa vya Aru na Tanah Besar. Mwaka wa 2011 idadi ya wasemaji wa Kibatuley imehesabiwa kuwa watu 3640. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibatuley iko katika kundi la Kiaru.