Kibedoanas ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wabedoanas kwenye kisiwa cha Papua. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kibedoanas imehesabiwa kuwa watu 180 tu. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibedoanas iko katika kundi la Kibomberai.