Kibembe

Kibembe ni lugha ya Kibantu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inayozungumzwa na Wabembe. Mwaka wa 1991 idadi ya wasemaji wa Kibembe nchini Kongo imehesabiwa kuwa watu 252,000. Pia kuna wasemaji nchini Tanzania. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kibembe iko katika kundi la D50.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne