Kibeng

Kibeng ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Cote d'Ivoire inayozungumzwa na Wabeng. Mwaka wa 1993 idadi ya wasemaji wa Kibeng imehesabiwa kuwa watu 17,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibeng iko katika kundi la Kimande.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne