Kibenga ni lugha ya Kibantu nchini Guinea ya Ikweta na Gabon inayozungumzwa na Wabenga. Mwaka wa 1995, idadi ya wasemaji ya Kibenga nchini Guinea imehesabiwa kuwa watu 3000; na mwaka wa 2004 idadi nchini Gabon imehesabiwa kuwa watu 1100. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kibenga iko katika kundi la A30.