Kiberti

Kiberti ilikuwa lugha ya Kinilo-Sahara nchini Sudan iliyozungumzwa na Waberti. Wakati wa miaka ya 1990, kulikuwa hakuna wasemaji wa Kiberti tena, maana yake lugha imetoweka kabisa kwa vile Waberti walibadilisha lugha yao na kuongea Kiarabu tu. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiberti iko katika kundi la Sudaniki-Mashariki.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne