Kibete-Gagnoa

Kibete-Gagnoa ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Cote d'Ivoire inayozungumzwa na Wabété. Isichanganywe na Kibete ya Nigeria. Mwaka wa 1989 idadi ya wasemaji wa Kibete-Gagnoa imehesabiwa kuwa watu 150,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibete-Gagnoa iko katika kundi la Kikru.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne