Kibisu ni lugha ya Kisino-Tibeti nchini Uthai inayozungumzwa na Wabisu. Mwaka wa 2016 idadi ya wasemaji wa Kibisu imehesabiwa kuwa watu 700, na wote hao pia huzungumza Kithai-Kazkazini. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kibisu iko katika kundi la Kingwi.