Kibodi (pia: Kiibodi[1], Kicharazio[2], Baobonye au Bodidota/Bodi ya dota[3]; kwa Kiingereza: keyboard) ni kifaa muhimu kinachomwezesha mtu kuweka maandishi na namba kwa tarakishi (kompyuta). Inafanywa na vibonye vingi kwa ajili ya kila herufi na alama nyingine zinazotumiwa mara kwa mara.
Kibodi ni pia sehemu ya chombo cha muziki k.v. piano, iliyo na vibonye vyenye rangi vinavyobonyezwa ili kutoa sauti.
Kwa tarakilishi nyingi ni kifaa kikuu cha kuingizia habari mashineni.
Kuna mifumo mbalimbali za baobonye kulingana na lugha.
Muundo wa kawaida kwa lugha zinazotumia alfabeti ya Kilatini ni QWERTY (hizi ni herufi 6 za kwanza).
Muundo huu unaweza kuchosha mikono na vidole. Ulianzishwa zamani za mashine za kupiga chapa na mfumo wa herufi ulilenga kutovurugisha mikono ya taipu. Siku hizi ni kama hakuna taipu tena, lakini watu waliozoea muundo umebaki vile.