Kibokyi

Kibokyi ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Nigeria inayozungumzwa na Wabokyi. Mwaka wa 1989 idadi ya wasemaji wa Kibokyi imehesabiwa kuwa watu 140,000. Pia kuna wasemaji 3700 nchini Kamerun. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibokyi iko katika kundi la Cross River.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne