Kibomitaba ni lugha ya Kibantu nchini Jamhuri ya Kongo inayozungumzwa na Wabomitaba. Mwaka wa 1982 idadi ya wasemaji wa Kibomitaba nchini Kongo imehesabiwa kuwa watu 9600. Pia kuna wasemaji 220 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kibomitaba iko katika kundi la C20.