Kibomu

Kibomu ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Mali na Burkina Faso inayozungumzwa na Wabomu. Mwaka wa 1976 idadi ya wasemaji wa Kibomu nchini Mali imehesabiwa kuwa watu 102,000. Pia kuna wasemaji 56,000 nchini Burkina. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibomu iko katika kundi la Kigur.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne