Kiboor ni lugha ya Kiafrika-Kiasia nchini Chad inayozungumzwa na Waboor. Mwaka wa 1999 idadi ya wasemaji wa Kiboor imehesabiwa kuwa watu 100 tu. Kwa hiyo lugha imekaribia kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiboor iko katika kundi la Kichadiki.