Kibudong-Budong

Kibudong-Budong (pia Kitangkou) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wabudong-Budong kwenye kisiwa cha Sulawesi. Mwaka wa 1989 idadi ya wasemaji wa Kibudong-Budong imehesabiwa kuwa watu 70 tu. Kwa vile watoto hawajifunzi lugha, Kibudong-Budong imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibudong-Budong iko katika kundi la Kisulawesi-Kusini.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne