Kibum

Kibum ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Kamerun inayozungumzwa na Wabum. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kibum imehesabiwa kuwa watu 21,400. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibum iko katika kundi la Grassfields ambalo linafanana na lugha za Kibantu.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne