Kiburuwai ni lugha ya Kivuka-Guinea Mpya nchini Indonesia inayozungumzwa na Waburuwai. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kiburuwai imehesabiwa kuwa watu 1000, lakini wengi wao wameanza kubadilisha lugha. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiburuwai iko katika kundi la Kisabakor.