Kibwisi (Gabon)

Kibwisi ni lugha ya Kibantu nchini Jamhuri ya Kongo na Gabon inayozungumzwa na Wabwisi. Isichanganywe na Kitalinga-Bwisi cha Uganda. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kibwisi imehesabiwa kuwa watu 3020 nchini Kongo na watu 1230 nchini Gabon. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kibwisi iko katika kundi la B40.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne