Kichin-Bawm

Kichin ya Bawm (au Kibawm) ni lugha ya Kisino-Tibeti nchini Bangladesh, Uhindi na Myanmar inayozungumzwa na Wachin. Mwaka wa 2011 idadi ya wasemaji wa Kichin ya Bawm nchini Bangladesh imehesabiwa kuwa watu 10,000. Pia kuna wasemaji 4400 nchini Uhindi (2004) na wasemaji 1500 nchini Myanmar (2010). Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kichin ya Bawm iko katika kundi la Kisal.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne