Kichin ya Paite (pia Kipaite) ni lugha ya Kisino-Tibeti nchini Uhindi inayozungumzwa na Wachin. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kichin ya Paite imehesabiwa kuwa watu 64,100. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kichin ya Paite iko katika kundi la Kisal.