Kichukwa

Kichukwa ni lugha ya Kisino-Tibeti nchini Nepal inayozungumzwa na Wachukwa. Mwaka wa 2011 idadi ya wasemaji wa Kichukwa imehesabiwa kuwa watu 100 ambao watano wao tu waliweza kuzungumza Kichukwa vizuri, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kichukwa iko katika kundi la Kihimalaya.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne