Kidawera-Daweloor ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wadawera na Wadaweloor kwenye visiwa vya Dawera na Daweloor. Mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kidawera-Daweloor imehesabiwa kuwa watu 1270. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kidawera-Daweloor iko katika kundi la Kibabar.