Kideg ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Ghana inayozungumzwa na Wadeg. Mwaka wa 2003 idadi ya wasemaji wa Kideg nchini Ghana imehesabiwa kuwa watu 26,400. Pia kuna wasemaji 1100 nchini Cote d'Ivoire. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kideg iko katika kundi la Kigur.