Kidhao (pia Kindau au Kikahore) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wadhao kwenye visiwa vya Ndau, Rote na Timor. Mwaka wa 1997 idadi ya wasemaji wa Kidhao imehesabiwa kuwa watu 5000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kidhao iko katika kundi la Kisumba-Hawu.