Kidigo

Kidigo (pia huitwa Chidigo) ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania na Kenya inayozungumzwa na Wadigo. Mwaka wa 1994 idadi ya wasemaji wa Kidigo nchini Kenya imehesabiwa kuwa watu 217,000. Pia kuna wasemaji 88,000 nchini Tanzania (1987). Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kidigo iko katika kundi la E70.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne