Kidongotono ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Sudan Kusini inayozungumzwa na Wadongotono. Mwaka wa 1978 idadi ya wasemaji wa Kidongotono imehesabiwa kuwa watu 1000 tu. Wataalamu wengine huiangalia kama lahaja ya Kiotuho. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kidongotono iko katika kundi la Kinilotiki.