Kidrung ni lugha ya Kisino-Tibeti nchini Uchina inayozungumzwa na Wadrung. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kidrung imehesabiwa kuwa watu 14,000. Pia kuna wasemaji 225 nchini Myanmar. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kidrung iko katika kundi la Kinungish.