Kidudu mataya-duni | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kidudu mataya-duni
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Kidudu mataya-duni (Limnognathia maerski) ni kidudu mdogo sana wa familia Limnognathiidae katika faila Micrognathozoa wanaoishi katika chemchemi za maji moto (±70ºC) kwenye Kisiwa cha Disko, Grinilandi[1]. Kwa kisasa ni spishi pekee ya familia na faila zake. Akiwa na urefu wa µm 100, ni mwongoni mwa wanyama wadogo kabisa duniani.
Anajilisha na bakteria, sianobakteria (“viani kijanibuluu”) na diatomu. Ana mataya tata sana yenye sehemu 15 tofauti zilizo duni sana (µm 4-14). Kidudu huyo anaweza kunyumbua mataya yake nje ya mdomo wake akila.
Spishi hii ina ganglioni kubwa ndani ya kichwa chake na jozi ya kamba za neva zinazoenda kupitia upande wa chini mpaka mkia. Ogani za fahamu ni nywele ngumu zilizoundwa kwa silio moja hadi tatu na kutawanyika mwilini kote. Silio kinamo ziko kwenye eneo la undo la kiatu cha farasi juu ya paji, kwenye mahali kadhaa kwa pande za kichwa na kwenye mistari miwili kwa upande wa chini wa mwili. Silio za paji husababisha mkondo wa maji unaosogeza chembe za chakula kuelekea mdomo. Silio nyingine husogeza kidudu.