Kiduma

Kiduma ni lugha ya Kibantu nchini Gabon inayozungumzwa na Waduma. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kiduma imehesabiwa kuwa watu 9840. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kiduma iko katika kundi la B50.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne