Kielelezo (pia: mfano au modeli kutoka Kiingereza mdel[1]) ni uwakilishi wa kina wa kitu, mtu au mfumo.
Modeli zinaweza kugawanywa katika modeli za kimwili (kama modeli ya meli au modeli ya mavazi) na modeli dhahania (mfano, seti ya milinganyo ya kihesabu inayoelezea jinsi angahewa linavyofanya kazi kwa madhumuni ya utabiri wa hali ya hewa). Modeli za dhahania au dhana ni muhimu sana katika falsafa ya sayansi.
Katika utafiti wa kitaaluma na sayansi inayotumika, modeli haipaswi kuchanganywa na nadharia: wakati modeli inalenga tu kuwakilisha uhalisia kwa madhumuni ya kuelewa au kutabiri ulimwengu vizuri zaidi, nadharia ina malengo makubwa zaidi kwa kudai kuwa ni maelezo ya uhalisia.