Kiembaloh

Kiembaloh (pia Kimalo, Kipalin au Kisanggau) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wataman, Wapalin, Wasuai, Walauk na Wakalis kwenye kisiwa cha Kalimantan. Mwaka wa 1991 idadi ya wasemaji wa Kiembaloh imehesabiwa kuwa watu 10,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiembaloh iko katika kundi la Kisulawesi-Kusini.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne